Wengine wataka kutumia matambara kujisitiri hedhi
Pakua
Suala la wanawake na wasichana kujisitiri wakati wa hedhi limesalia kuwa kizungumkuti hasa katika nchi maskini zijulikanazo pia kama nchi zinazoendelea. Hii ni kutokana na kwamba katika jamii nyingi za maeneo hayo suala hilo ni mwiko kuzungumzwa hadharani na pia pedi za kisasa ambazo hazina madhara ya kiafya ni vigumu kuzimudu kwa kuwa ni ghali. Hii inawalazimu baadhi ya wazazi kuwashauri watoto wao kutumia nguo kuukuu kujisitiri kama njia mbadala. Lakini hilo madaktari wanasema halifai. Kupambanua mvutano huo Siraj Kalyango anakualiaka kwenye Makala hii.
Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
3'59"