Nachukizwa sana na wanaoona wenye shida ni ombaomba- Brenda

Nachukizwa sana na wanaoona wenye shida ni ombaomba- Brenda

Pakua

Kwa siku nne kuanzia tarehe 8 Februari 2018 vijana kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikutana jijini New York, Marekani kwa ajili ya mjadala wa mustakhbali wa dunia. Mjadala huo wa vijana umefanyika kwa kuzingatia mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwandaa vijana kubeba jukumu la kusongesha maendeleo kwenye nchi zao na dunia kwa ujumla. Miongoni mwao ni Brenda Kimwatan, mwanafunzi kutoka Kenya ambaye anasoma Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini. Katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Brenda ametupatia taswira ya kilichofanyika na matarajio ya baadaye. Lakini kwanza anaanza na ilikuwaje hadi akapita kinyang’anyiro cha kuwakilisha chuo chake.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman