Wachuuzi wa samaki Burundi na mafunzo ya kuepusha uchafuzi wa mazingira
Ziwa Tanganyika kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika, limekuwa mashuhuri sio kwa kusafirisha watu na bidhaa bali pia katika kuzalisha samaki aina mbalimbali Lakini changamoto kubwa ni uhifadhi za samaki baada ya kuvuliwa hadi kuliwa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira. Ingawa samaki huonekana kwa wengi kama chakula bora, lakini kama hawatahifadhiwa vyema wanaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji na mazingira. Hivi karibuni , wavuvi na wauzaji wa samaki mjini Bujumbura nchini Burundi walihamasishwa jinsi ya kuhifadhi vyema samaki kwa matumizi ya mlo lakini pia kuhakikisha wanahifadhi mazingira kwa kutotupa hovyo samaki walioharibika.. Katika makala hii mwandishi wetu wa maziwa Makuu Ramadhani Kibuga amezungumza na wachuuzi wa samaki sokoni CoTeBu ili kufahamu mbinu wanazotumia kuhifadhi samaki wao.