Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki ni daraja la ushirikiano kwa watoto wakimbizi

Muziki ni daraja la ushirikiano kwa watoto wakimbizi

Pakua

Sanaa ya Muziki hutumika kama chombo cha ushirikiano wa kijamii na imeleta nuru kwa watoto na vijana wakimbizi wanaosaka hifadhi nchini Sweden.  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la El Sistema wameandaa tamasha la muziki huko Stockholm linaloleta pamoja wakimbizi kutoka Syria, Afghanistan, Eritrea, Albania, Venezuela na wenyeji wa Sweden. Wengi wa watoto katika bendi hii hawajawahi kucheza ala yoyote ya muziki kabla ya kujiunga na wasanii hao wa muziki hao.  Kulikoni? Ungana na Selina na Jerobon..

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
3'52"
Photo Credit
UNHCR/Caroline Bach