Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi anatafuta maisha - JJ Bola

Mkimbizi anatafuta maisha - JJ Bola

Pakua

Umoja wa Mataifa unaendelea kusisitiza kuwa mtazamo potofu kuhusu uhamiaji na wahamiaji umeendelea kukwamisha matumizi bora ya dhana hiyo kote ulimwenguni. Umoja huo unahimiza serikali zote kuenzi mbinu tofouti za kufanya uhamiaji uwe na manufaa kwa wote, maana wakimbizi wanaweza kuchangia katika uchumi ya nchi wanamoishi. Licha ya wito huo bado wakimbizi wengi bado wanapitia machungu wanapokuwa ukimbizini, kitu ambacho kinasababisha wengi kuwaza walikotoka na machungu walioyapitia. Katika makala ifuatayo, Selina Jerobon kwa mchango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anakutana na mkimbizi  JJ Bola ambaye pia ni Msanii wa ushairi.  Je ametumia ushairi kupitisha ujumbe gani? Ungana naye….

Audio Credit
UNHCR/JJ Bola
Audio Duration
3'55"
Photo Credit
Wakimbizi wajasiriamali wa Mali walioko nchini Burkina Farso. Picha: UNHCR/Video capture