Kazi ni kazi , ukiitilia maanani:
Shirika la la kazi duniani ILO, linesema ukosefu wa ajira kwa vijana bado ni changamoto kubwa duniani kote. Umoja wa Mataifa na mashirika yake wamekuwa mstari wa mbele kuhimiza serikali na asasi za kiraia kutoa mafunzo yatakayowezesha vijana kujiajiri ili kuepuka zahma ya kutokuwa na ajira.
Katika taaluma za kiufundi moja ya mbinu ya kuzifunza kazi kwa baadhi ya vijana ni kupata fursa ya kijifunza taaluma kupitia kwa wazazi wao. Vijana wengi wamejikuta wamerithi kazi za babu, baba zao, mama au ndani ya familia.
Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA akiwa mjini Bujumbura Burundi amekutana na kijana SALUM HAMISI aliyerithi kazi ya kunyoosha na kutengeneza magari kutoka kwa baba yake. Nini anachokifanya Salum? Ungana na Ramadhani