Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa wanawake katika kuchagiza amani Kenya

Mchango wa wanawake katika kuchagiza amani Kenya

Pakua

Mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW63 unafunga pazia leo Machi 22 hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huu ambao umewaleta pamoja zaidi ya washiriki 9000 kutoka wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa umoja huo pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya kiraia umejadili  jinsi gani mwanamke ataweza kukombolewa katika suala zima la uongozi lakini vilevile kumpatia mwanamke uwezo wa kuongeza mchango wake katika jamii.

Mkutano huo umetoa mapendekezo ambayo ungetaka yafanyike ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kisheria na mazingira ya taasisi hizo, kukabiliana na pengo la kijinsia na chuki za masuala ya  kijinsia katika ulinzi wa jamii, kubadili huduma za umma kwa ajili ya kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, kuhakikisha uwekezaji wa miundombinu unazingatia mahitaji ya wanawake na wasichana, kuchangisha raslimali ,uwajibikaji na ushahidi.

Kwa upande wa wanawake iwe katika serikali au mashirika ya kiraia wamepata ari mpya baada ya kutoa hotuba kuhusu hali ya mwanamke katikanchini zao lakini pia kwa kusikiliza simulizi kutoka nchi mbali mbali. Miongoni mwa wanawake ambao wamehudhuria mkutano huo ni kutoka Kenya  ni Bi Ida Odinga mwenyekiti wa kikundi cha kusongesha harakati za kuleta amani kwa jina la Embrace.

Na bi Rachel Shebesh katibu tawala kwenye wizara ya maswala ya jinsia, wazee na watoto Kenya ambaye pia ni mwanachama wa Embrace. Wamezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii ambapo kwanza Bi Odinga anaelezea mambo yanayochangia kuwepo na pengo la usawa wa kijinsi nchini mwake.

(MAHOJIANO PKG)

 

Audio Credit
Patrick Newman
Sauti
5'54"
Photo Credit
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya