Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuo cha BareFoot chaleta mabadiliko kwa wanawake Zanzibar

Chuo cha BareFoot chaleta mabadiliko kwa wanawake Zanzibar

Pakua

Leo katika makala yetu Flora nducha wa Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Pendo Yeredi Daudi Mratibu wa chuo cha Bearfoot kilichoanziswa na serikali ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanawake wa vijijini huko visiwani Zanzibar, mafunzo ambayo yamekuwa mkombozi mkubwa kwao. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya mradi wa kutengezeza paneli za nishati ya jua au sola. Mradi huo unaendeshwa na wanawake tu tena wa vijijini maarufu kama sola mamamazi , umeleta tija kwa wanawake hao, familia zao na jamii kwa ujumla.

Kwa undani zaidi kuhusu mradi huo ungana na Flora na Pendo anayeaanza kwa kufananua mbinu  za kitaalam wanazozitumia chuoni kuwafundishia wanawake hao ambao hawakubahatika kwenda shule.

Audio Credit
PATRICK NEWMAN /FLORA NDUCHA / PENDO DAUDI
Audio Duration
5'49"
Photo Credit
Shutterstock