Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Fistula bado tatizo, UNFPA Tanzania wapania kuitokomeza

Fistula! Ugonjwa unaowakumba wanawake na wasichana kutokana na kuchelewa kupata huduma stahiki wakati wa kujifungua. Takwimu zinaonyesha kuwa licha ya mafanikio katika mbinu za kisasa za kutoa huduma ya afya bado takriban wanawake 800 wanafariki dunia kutokana na maradhi yatokanayo na uja uzito kila siku na kwa kila mwanamke anayefariki takriban wanawake 20 wanapata majeraha ya maisha kama vile fistula.

Wadau wote wanapaswa kushiriki vita dhidi ya ukeketaji:UNFPA

Nchi mbalimbali zimekuwa zikichukua hatua ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma, na wadau wote wakiwemo mangariba.

Kampeni kubwa inafanywa na shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA inayosistiza kwamba wadau wote katika jamii ikiwemo serikali , viongozi wa dini na mangariba wanapaswa kushiriki vita hivi.

Florence Gachanja ni afisa mipango wa UNFPA Kenya amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii na anaanza kwa kufafanua hali ya tatizo hili nchini Kenya.

(MAHOJIANO NA  FLORENCE)

Vijana wajiongeze ili kushika fursa za kiuchumi na kisiasa: Francine Muyumba #Youth2030

Barani Afrika, vitisho vya kigaidi kutoka vikundi vya waasi kama vile Boko Haram nchini Nigeria au ADF-Nalu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC vimesababishwa na vijana wa maeneo hayo kukataa tamaa na kukosa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Hayo ni maoni ya Francine Furaha Muyumba ambaye ameshiriki Kongamano la vijana lililofanyika wiki hii mjini New York, Marekani na kujumuisha wawakilishi zaidi ya 800 na mawaziri 21 kutoka nchi mbali mbali wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Vita dhidi ya vikundi vya misimamo mikali ni lazima vianzie mashinani:Dkt. Ali

Februari mosi hadi saba ni wiki ya kuadhimisha  uwiano baina ya imani mbalimbali za kidini ulimwenguni. Wiki hii ilitengwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio la tarehe 20 Oktoba mwaka 2010. Azimio hilo pamoja na mambo mengine linataja uelewa na mazungumzo baina ya dini mbalimbali kama kiungo muhimu katika kuimarisha maelewano miongoni mwa watu wengi licha ya Imani zao.

Fahamu utamaduni wa dansi India

Utamaduni ni maisha, ndivyo unavyoweza kusema ukiwa unatafakari na kuzingatia uatamaduni wa watu wa India ambapo pamoja na mambo mengine utamaduni wa jamii moja ya watu wa India ambao hucheza na nyoka huwashangaza wengi. Shirika la Umoja la Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO linapigia chepuo utamduni huu ambao uko hatarini kutoweka.

Ungana na Amina Hassan katika makala itakayopeleka nchini India huku pia ukijifunza utamaduni jadilifu wa nchi hiyo.

Nishati mbadala nchini Uganda

Upatikanaji wa nishati kwa wote ni changamoto kwa karne ya 21, wakati ambapo mtu mmoja kati ya watano hawapati huduma za umeme duniani, na Umoja wa Mataifa ukitarajia kuwa mahitaji ya nishati yataongezeka kwa asilimia 33 ifikapo mwaka 2035.

Miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs yaliyopitishwa mwaka 2015, lengo namba 7 ni kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote na kwa bei nafuu.

Mwelekeo wa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania watia matumaini- UNFPA

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango imeonyesha ongezeko katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania. Takwimu zinasema kuwa matumizi sasa ni asilimia 27 ya watanzania wenye uwezo wa kutumia njia hizo ikiwemo sindano, vipandikizi na mipira ya kiume na ya kike.

Lakini ni hatua gani ambazo zimechangia ongezeko hilo japo linaelezwa kuwa ni la wastani? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Felister Bwana, Afisa programu wa afya ya mama na mtoto kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu, UNFPA nchini humo.

Mwelekeo wa uwekezaji wa kigeni Afrika watia shaka 2016- UNCTAD

Ripoti mpya ya kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu mwelekeo wa uwekezaji wa vitegauchumi wa kigeni duniani imeonyesha bayana kuzidi kudidimia kwa uwekezaji huo katika nchi za Afrika hususan zile zinazoendelea. Hata hivyo mataifa mengine yamenufaika kwa kupata uwekezaji mkubwa ambapo kwa ujumla yaelezwa kuwa uwekezaji huo duniani umeongezeka kwa asilimia 36 mwaka 2015. Je kwa ni nchi zipi zimenufaika zaidi? Sababu ni nini? Na mwelekeo ni upi unatarajiwa? Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt.

Usalama wa chakula CAR shakani

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati machafuko yamesababisha hali tete ya usalama wa chakula na hivyo kuongeza kadhia kwa raia wa nchi hiyo mjini na vijijini.

Watoto wanakumbwa na hatari ya utampiamlo huku afya ya jamii kwa ujumla ikizorota. Ungana na Grace Kaneiya katika makala inayofafanua madhila hayo na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kutoa usaidizi.