Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

16 Mei 2022

Katika jarida la Jumatatu Mei 16, 2022 na Leah Mushi

Mradi wa mafunzo wa ILO wawainua wafanyabiashara Turkana magharibi, Kenya

UNMAS yaendelea kunusuru maisha ya watu Sudan Kusini kwa kutegua mabomu ya kutegwa ardhini

 

Makala ni kutoka Dar es Salaam Tanzania ambako Philbert Alexander wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa ameingia katika mitaa ya Dar es Salaam kuzungumza na baadhi ya wasichana na wanawake kuhusu namna wanavyouelewa usawa wa kijinsia.

Sauti
12'52"

13 Mei 2022

Katika jarida hii leo utasikia wito wa kusaidia wakulima wa Somalia ili kuiokoa nchi isiingie katika janga kubwa la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linatumia wafanyakazi wa kijamii kuhamasisha wakazi wa vitongoji vya mji mkuu, Kinshasa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona, au COVID-19 kwa kuwa baadhi ya watu bado wanasuasua kupatiwa chanjo hiyo.

Wananchi wa Turkana Kenya wamepaaza sauti ya madhila yanayowasibu na UNICEF kueleza nini wanafanya kusaidia katika eneo la usafi na kujisafi. 

Sauti
12'58"

12 Mei 2022

Jaridani Alhamisi Mei 12, 2022 na Grace Kaneiya HABARI KWA UFUPI Mratibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masauala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths yuko ziarani nchi Kenya kwa lengo la kuitanabaisha jumuiya ya kimataifa janga la kibinadamu lililosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika Pembe ya Afrika, nchini Ethiopia, Somalia na Kenya. Zaidi ya watu milioni 15 hawana uhakika wa chakula kutokana na ukame mkali ambapo Kenya pekee watu milioni 3.5 wanakabiliwa na njaa huku viwango vya utapiamlo vikiongezeka mara mbili.
Sauti
12'37"

11 Mei 2022

Katika jarida hii leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID limesema ingawa bara la afrika limepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya janga la COVID-19, idadi ya wagonjwa na vifo inapungua lakini bado kuna changamoto kubwa kuhusu janga hilo.

Sauti
13'12"

10 Mei 2022

Hii leo jaridani siku ya Jumanne ni Mada kwa Kina na tunakupeleka Kenya kufuatilia majaribio ya chanjo dhidi ya Malaria na mwenyeji wetu huko ni Thelma Mwadzaya. Lakini kuna habari kwa ufupi tukimulika Syria, Ukoma na matumizi ya mtandao katika kuuza pombe kutoka nchi moja hadi nyingine. Mashinani tunakwenda Moldova, karibu na anayekusomea jarida la leo ni Grace Kaneiya.

Sauti
11'41"

09 Mei 2022

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO na shirika la kiraia liitwalo COMOA wameshirikiana kuimarisha usalama Goma, DRC.

Mradi wa Merankabandi wa UNICEF Burundi na Benki ya Dunia wanufaisha wanajamii.

Makala tutaelekea Sudan na upande wa mashinani kuangazia namna mradi wa kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na wanawake umeleta mabadiliko katika jamii.

Sauti
12'23"

5 Mei 2022

Jaridani Alhamisi Mei 5, 2022 na Leah Mushi

Mradi wa maji DRC wapunguza maambukizi ya Kipindupindu

Wakimbizi na jamii zinawazowahifadhi Bogo Cameroon wanahitaji kujengewa mnepo:UNHCR

Wadau wa Sekta ya Habari barani Afrika wamekutana jijini Arusha nchini Tanzania kujadili na kutoa mapendekezo mapya ili kuboresha Mpango wa Utekelezaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usalama wa Waandishi wa Habari uliotengenezwa miaka 10 iliyopita.

Sauti
14'56"

4 Mei 2022

Jaridani Jumatano Mei 4, 2022 na Leah Mushi

Kwanza ni habari kwa ufupi-

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehitimisha ziara yake ya siku 4 katika nchi tatu za Afrika Magharibi, kwa kutembelea Nigeria, baada ya kuzuru pia Senegal na Niger. Akiwa Borno, jimbo la Nigeria ambalo mara kwa mara limekumbwa na mashambulizi ya kigaidi, Guterres amesema, "watu niliokutana nao leo wanataka kurudi nyumbani kwa usalama na utu.

=============================================  

Sauti
12'5"

Mei 3 2022

Jaridani Mei 3, 2022 na Leah Mushi-

-Udukuzi wa kidijitali na kuwanyamazisha kisiasa ni tishio kwa waandishi wa habari: UN

-MINUSCA yazindua kampeni ya kusaidia upatikanaji wa amani CAR

-Watoto milioni 10 wako hatarini kutokana na ukame Pembe ya Afrika:UNICEF

-Kwenye makala ni ziara katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa iliyofanywa na mwanamuziki kutoka Nigeria na mshindi wa tuzo ya Grammy, Burna Boy.

Sauti
13'