Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

4 Mei 2022

4 Mei 2022

Pakua

Jaridani Jumatano Mei 4, 2022 na Leah Mushi

Kwanza ni habari kwa ufupi-

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehitimisha ziara yake ya siku 4 katika nchi tatu za Afrika Magharibi, kwa kutembelea Nigeria, baada ya kuzuru pia Senegal na Niger. Akiwa Borno, jimbo la Nigeria ambalo mara kwa mara limekumbwa na mashambulizi ya kigaidi, Guterres amesema, "watu niliokutana nao leo wanataka kurudi nyumbani kwa usalama na utu.

=============================================  

Mtandao wa kimataifa duniani dhidi ya janga la chakula, GNAFC umezindua ripoti yake hii leo huko Roma, Italia kuhusu janga la chakula inayosema kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula sambamba na wanaohitaji siyo tu msaada wa chakula kuokoa maisha yao bali pia msaada wa kuendesha maisha yao inaongezeka kwa kiasi kinachotia mashaka makubwa. 

============================================  

Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, na mtandao wa  TikTok wameungana leo kuzindua kampeni ya muziki inayohimiza mshikamano na wakimbizi duniani kote. 

Kwenye mada kwa kina makala kuhusu jukwaa la watu wa asili na kijana kutoka jamii ya Endorois ya Kenya.

Katika mashinani tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'5"