Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Mei 2022

11 Mei 2022

Pakua

Katika jarida hii leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID limesema ingawa bara la afrika limepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya janga la COVID-19, idadi ya wagonjwa na vifo inapungua lakini bado kuna changamoto kubwa kuhusu janga hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Uganda linaendesha programu ya waelimishaji rika ambayo imesaidia watoto kadhaa wa kike akiwemo Sara kuacha kujiua baada ya kubakwa na kupewa ujauzito na hatimaye kurejea shuleni kusoma huku akilea mtoto wake na kuwa na matarajio makubwa kwa siku za usoni.

kwa undani wa taarifa hizo na makala kutoka DRC na Mashinani kutoka Papua New Guinea karibu usikilize jarida

 

Audio Credit
Grace kaneiya
Audio Duration
13'12"