Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 Mei 2022

13 Mei 2022

Pakua

Katika jarida hii leo utasikia wito wa kusaidia wakulima wa Somalia ili kuiokoa nchi isiingie katika janga kubwa la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linatumia wafanyakazi wa kijamii kuhamasisha wakazi wa vitongoji vya mji mkuu, Kinshasa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona, au COVID-19 kwa kuwa baadhi ya watu bado wanasuasua kupatiwa chanjo hiyo.

Wananchi wa Turkana Kenya wamepaaza sauti ya madhila yanayowasibu na UNICEF kueleza nini wanafanya kusaidia katika eneo la usafi na kujisafi. 

Audio Credit
Grace kaneiya
Audio Duration
12'58"