Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

5 Mei 2022

5 Mei 2022

Pakua

Jaridani Alhamisi Mei 5, 2022 na Leah Mushi

Mradi wa maji DRC wapunguza maambukizi ya Kipindupindu

Wakimbizi na jamii zinawazowahifadhi Bogo Cameroon wanahitaji kujengewa mnepo:UNHCR

Wadau wa Sekta ya Habari barani Afrika wamekutana jijini Arusha nchini Tanzania kujadili na kutoa mapendekezo mapya ili kuboresha Mpango wa Utekelezaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usalama wa Waandishi wa Habari uliotengenezwa miaka 10 iliyopita.

Makala ni mradi wa Dreams unaolenga kutoa elimu ya afya ya uzazi na kujikinga na magonjwa hususani kwa vijana balehe mkoani Mbeya, Tanzania.

Mashinani ni tunamsikia muhudumu wa afya Macron Chauluka aliye mstari wa mbele kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo dhidi ya polio Malawi kupitia program ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na anatembela kilometa 3 kila siku ili kutimiza azma yake ya kutoa chanjo.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
14'56"