Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

April 29 2022

April 29 2022

Pakua

Karibu kusikiliza jarida hii leo ambapo utapata fursa ya kusikiliza makala ya athari za Mafuriko kwenye sekta ya elimu nchini Uganda na kujifunza kiswahili, leo ufafanuzo wa methali Umejigeuza Pweza kujipalia Makaa umetolewa

 

Pamoja na hayo utapata fursa ya kusikiliza taarifa ya habari kwa ufupi ambapo

- Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO imefichua kiwango cha kushtua cha soko au uuzaji wa kinyonyaji wa maziwa ya mtoto yanayotegenezwa viwandani. 

-WHO pia imetoa dola za Kimarekani milioni 8.3 kutoka katika Ufadhili wake wa Dharura kusaidia watu milioni 10.6 wanaohitaji huduma za dharura za afya katika eneo la Sahel barani Afrika. 

- Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine  44 wa misaada ya kibinadamu wametoa ombi la dharura la dola za Marekani milioni 47.8 ili kukabiliana na mahitaji muhimu ya maelfu ya wakimbizi waliofika Uganda mwaka huu, wakikimbia ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'52"