Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 Aprili 2022

22 Aprili 2022

Pakua

Hii leo Jaridani mwenyeji wako ni Grace Kaneiya akikuletea jarida limesheheni mada kwa kina, Habari kwa Ufupi na kujifunza kiswahili.

Mada kwa kina ni uzinduzi wa filamu ya Royal  Tour Tanzania uliofanyika hapa Marekani na tunamulika mchango wake katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDG na mchambuzi ni Gerson Msigwa, Msemaji wa serikali ya Tanzania. 

Habari kwa Ufupi zinaanzisha hapa Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres na ujumbe wake wa siku ya Mama Sayari Dunia. Je nini kifanyike kulinda makazi haya pekee tuliyojaliwa? Na kisha anamulika malazi mapya kwa wakimbizi wa ndani Ukraine na Habari kwa Ufupi inafungwa na taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuhusu doria za walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Malawi.

Na katika kujifunza kiswahili hii leo tunasalia Tanzania kwake Onni Sigalla na uchambuzi wa neno “nyunyuta,” Karibu!
 

Audio Credit
GRACE KANEIYA
Audio Duration
12'47"