Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 Aprili 2022

25 Aprili 2022

Pakua

Jarida la Jumatatu Aprili 25 kwanza ni habari kwa ufupi-

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umelaani vikali unyanyasaji na ukatili wa kingono ulioenea, mauaji ikiwa ni pamoja na watu kukatwa vichwa, kuchomwa moto raia wakiwa hai, na mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu katika Kaunti ya Leer.  

============================

Leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba maudhui “Tumia ubunifu ili kupunguza mzigo wa ugonjwa wa malaria na kuokoa maisha”. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO hakuna chombo kimoja kinachopatikana leo duniani ambacho kitatatua tatizo la malaria hivyom shirika hilo linataka uwekezaji na uvumbuzi utakaoleta mbinu mpya za kudhibiti vijidudu, uchunguzi, dawa za malaria na zana zingine ili kuharakisha kasi ya maendeleo dhidi ya kutokomeza ugonjwa huo wa malaria. 

=============================

Na jukwaa la 21 la Umoja wa Mataifa la watun wa asili, leo limefungua pazia jijini New York Marekani. Jukwaa hilo linalofanyika ana kwa ana na kwa njia ya mtandao likiwaleta pamoja watu kutoka kila pembe ya dunia mwaka huu linajikita na maudhui “Watu wa asili, biashara, uhuru na msingi wa haki za binadamu wanazostahili ikiwa ni pamoja na ya ridhaa kabla na baada ya taarifa”. 

MADA KWA KINA:

Ikiwa ni siku ya Malaria Duniani  mada kwa kina leo inaangazia Malaria kuhusu mbinu mpya za kudhibiti ugonjwa huo ikiwememo chanjo na utafiti wa matumizi ya Toxorhynchites aina ya mbu ambaye anakula mbu wengine hususan mbu aina ya Anopheles ambaye anaeneza ugonjwa wa Malaria.

Mwenyeji wako leo ni Leah Mushi.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'32"