Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 19 Januari 2022

Jarida 19 Januari 2022

Pakua

Kama ilivyo ada ya kila Jumatano tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunaangazia namna mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, ulivyogeuza maskini wa mjini huko Misri kuweza kukimu maisha vijijini kwa staha. 

Katika habari nyingine, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdullah Shahid ametoa hotuba yake ya vipaumbele vya kazi kwa mkutano huo wa 76 wa Baraza Kuu ambapo ametaja vipaumbele vikuu vitano vya kutekeleza katika mwaka huu 2022.  

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limeingia makubaliano ya muda mrefu au LTA na wasambazaji katika ununuzi wa dawa mpya ya kutibu ugonjwa wa Corona, au coronavirus">COVID-19 Molnupiravir. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa mwezi uliopita wa Desemba mwaka 2021 wa mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani, FDA ya kuruhusu dawa hiyo ianze kutumika kwa dharura katika matibabu ya baadhi ya wagonjwa wa coronavirus">COVID-19.  

Na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limesema ajira zilizotoweka nchini Afghanistan kufuatia ambadiliko ya utawala mwezi Agosti mwaka jana wa 2021 zilifikia zaidi ya nusu milioni kwenye robo ya tatu ya mwaka jana na makadirio ni kwamba kiwango hicho kinaweza kufikia laki tisa katikati ya mwaka huu wa 2022. “kusinyaa kwa fursa za ajira kwa asilimia 14 ifikapo katikati ya mwaka huu ni taswira halisi ya idadi ya wafanyakazi walioondolewa kwenye ajira kutokana na mabadiliko ya utawala sambamba na janga la kiuchumi linaloshamiri pamoja na vikwazo dhidi ya wanawake kufanya kazi.” Imeeleza taarifa ya ILO iliyotolewa leo Bangkok, Thailand.  

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'52"