Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 24 Januari 2022

Jarida 24 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo katika habari za Umoja wa Mataifa 


Ikiwa leo ni siku ya elimu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la coronavirus">COVID-19 na changamoto nyingine zinazokabili dunia hivi sasa zimedhihirisha umuhimu wa kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa.


Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limesema kiwango cha hasara wanayopata watoto kielimu kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa elimu kulikosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 ni vigumu kurekebishika.


Mkurugenzi Mkuu wa shirika na Afya la Umoja wa Mataifa, WHO hii leo ametaja vipaumbele vitano kwa ulimwengu na kwa WHO.


Na kwa upande wa mada kwa kina tunaelekea nchini Uganda kuangazia fursa na changamoto zilipopo baada ya shule kufunguliwa miaka miwili baada ya kufungwa ktuokama na mlipuko wa COVID-19.
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'44"