Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 26 Januari 2022

Jarida 26 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo


Mwenyekiti wa Bodi ya Ubia wa Elimu Duniani, GEP, Jakaya Kikwete azungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kueleza wanachofanya kuboresha mifumo ya elimu duniani. Ni baada ya kukutana na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa lengo la kujadili mustakabali wa mifumo ya elimu kwa nchi maskini.


Kuelekea siku ya kimataifa ya kukumbuka waathirika wa mauaji ya maangamizi au Holocaust inayoadhimishwa kesho Januari 27, wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kupambana na aina zote za chuki dhidi ya wayahudi lazima ibaki kuwa kipaumbele cha kimataifa ili kukabili chuki inayoongezeka.


Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesema utafiti uliofanywa katika nchi 17 katika kanda za Afrika, Amerika Kusini na Karibea umetoa taarifa mpya zinazoonesha kuwa huduma mbovu za afya unaongeza changamoto kwa wasichana na wanawake wanaokabiliwa na matatizo ya utoaji mimba usio salama. 


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO leo limekaribisha mchango mkubwa wa dola milioni 65 kutoka kwa Benki ya Maendeleo ya Asia, ADB utakaosaidia pamoja na mambo mengine upatikanaji wa chakula maeneo ya vijini nchini Afghanistan. 


Na mashinani tunaangazia tamko la Katibu Mkuu kuhusu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso. Karibu!
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'15"