Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 20 Januari 2022

Jarida 20 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa 

Programu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA kufundisha masuala ya haki za binadamu katika shule za watoto wakimbizi wa kipalestina katika ukanda wa Gaza, imesaidia siyo tu wanafunzi kutambua haki zao bali pia walimu ambao wanawafundisha na hivyo kusaidia katika kusongesha amani kwenye eneo ambalo hugubikwa na migogoro. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linasema, mwaka huu wa 2022, hali ni tete zaidi kwa kuwa Lebanon nayo nyenyewe imetwama kwenye janga la kiuchumi, hali iliyosababisha na wakimbizi nao kuwa katika hali ya umaskini uliokithiri. 

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBATT-5 kwenye ujumbe wa umoja huo unaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, kando mwa jukumu lao la ulinzi wa raia wamechukua jukumu la kusambaza huduma za maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo ambako wanalinda amani. 

Na mashinani tunaye mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya uhandisi wa kilimo nchini Malawi ambaye sasa yuko kwenye Chuo cha mafunzo ya takwimu na ndege zisizo na rubani au drones. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
12'4"