Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 28 Januari 2022

Jarida 28 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo 

Jamii ya Maasai tarafa ya Liliondo, Wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha kaskazini mwa Tanzania waanza kuamia katika shughuli ngeni kwao, kilimo baada ya shughuli yao ya kitamaduni yaani ufugaji, kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. 

Tathmini mpya ya uhakika wa upatikanaji wachakula, iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula duniani WFP, inaonesha karibu asilimia 40 ya wakazi wa Tigray nchini Ethiopia wanakabiliwa na ukosefu wa chakula uliokithiri ikiwa ni miezi 15 tangu kuanza kwa migogoro katika eneo hilo.  

Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameitaka jumuiya ya kimataifa kuzidisha shinikizo kwa jeshi la Myanmar ili likomeshe kampeni yake ya ukatili dhidi ya watu wa Myanmar na kusisitiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia mara moja.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietha Fore amesema pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Covid-19 na hasa mnyumbuliko wa hivi karibuni, Omicron, hakupaswi kuwa na visingizo, shule zinapaswa kubaki zikiwa zimefunguliwa kwani watoto hawaewzi kusubiri.   

Na katika kujifunza Kiswahili tunapata ufafanuzi wa msemo ‘Leo ni le msema kesho ni muongo’.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'34"