Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 21 Januari 2022

Jarida 21 Januari 2022

Pakua

Machache kati ya mengi kutoka Umoja wa Mataifa  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amelihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani na kutaja maeneo makuu matano ya vipaumbele vyake ambayo yanahitaij hatua za dharura ili kuweza kukabili changamoto zinazokabili Dunia hivi sasa. Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Profesa Kennedy Gastorn anachambua maana ya tukio hili. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema wakimbizi wa Eritrea walioko jimboni Tigray nchini Ethiopia wameelezea mazingira magumu wanayoishi kutokana na misaada kushindwa kuwafikia kwa muda mrefu kwa sababu ya ukosefu wa usalama  

Na timu ya wanasayansi iliyokuwa imetumwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kufanya utafiti baharini imebaini moja ya miamba nadra na kubwa zaidi wa matumbawe karibu na Tahiti huko bahari ya Pasifiki.  

Katika kujifunza Kiswahili, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, la Zanzibar, BAKIZA, Dkt.Mwanahija Ali Juma anafafanua maana ya methali "Lina na Fila havitangamani.”  

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'50"