Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 25 Januari 2022

Jarida 25 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo katika habari za Umoja wa Mataifa


Familia za wakimbizi wa ndani pamoja na zile zilizowakaribisha wakimbizi hao katika ukanda wa mashariki ya kati kwa sasa zinakabiliana na baridi kali kutokana na kuanguka kwa theluji wakati huu wanaishi kwenye mahema.


Msimu wa upanzi wakati wa majira ya chipukizi ukiwa unakaribia huko nchini Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limepatia wakulima mgao wa mbegu bora za ngano ili kuepusha njaa ilIyowakumba mwaka jana kutokana na kuchelewa kupanda mbegu bora wakati wa msimu wa baridi kali.


Luteni Jenerali Shailesh Tinaikar raia wa India ambaye anastaafu wadhifa wake kama Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS amewashukuru askari walinda amani waliokuwa chini yake hususani wanawake ambao anasema wanafanya kazi katika mazingira yenye changamoto zaidi.


Na mashinani tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi wanajamii walijitolea kuhakikisha wanatokomeza Ebola.
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'54"