Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 27 Januari 2022

Jarida 27 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu. 


Mnyumbuliko wa hivi karibuni wa virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19, Omicron ukiwa umesambaa ulimwenguni kote, ukosefu wa usawa wa chanjo unaweka baadhi ya watu hatarini zaidi kuruhusu minyumbuliko kubadilika na kuathiri wanadamu wengine. Afrika ina idadi ya chini zaidi ya watu waliochanjwa dhidi ya COVID-19 duniani lakini nchini Malawi mradi bunifu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kusambaza chanjo kwa njia ya gari unaongeza upatikanaji wa chanjo na imani ya chanjo miongoni mwa wanawake wajawazito katika jamii za vijijini.


Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shaka na shuku kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 zimekuwa chanzo cha kusuasua kwa kazi ya utoaji wa chanjo katika taifa hilo la Maziwa Makuu lakini harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF za kuhamasisha wanachi zinaendelea kuzaa matunda na hata wale waliokuwa wanapinga sasa wanakubali kupatiwa chanjo.


Katika makala tunamsikiliza Azziad Nasenya mcheza filamu ambaye ni kijana mwenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya.


Na mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika wa mauaji ya maangamizi tunasikia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Karibu!
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'8"