Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 31 Januari 2022

Jarida 31 Januari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo kutoka Umoja wa Mataifa 

Wakimbizi wa Burundi walioishi kwa vipindi tofauti na hata miongo kadhaa ukimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameanza kurejea nyumbani Burundi. Kundi la kwanza katika mwaka huu wa 2022 waeleza furaha yao kurejea nchini mwao.  

Shirika la UNAIDS limeeleza kuwa katika maambukizi mengi mapya 150,000 ya Virusi Vya UKIMWI miongoni mwa wa watoto katika mwaka 2020 yangeweza kuzuiwa. UNAIDS inasema maambukizi ya watoto 65,000 yalitokea mwaka wa 2020 kwa sababu wanawake ambao tayari wanaishi na VVU hawakutambuliwa wakati wa ujauzito na hawakuanza matibabu. Zaidi ya maambukizi 35,000 ya ziada ya watoto yalitokea kwa sababu wanawake walipata VVU wakati wa ujauzito au kunyonyesha, ambayo ilisababisha kuongezeka kwa kiwango cha virusi vyao na hatari kubwa ya maambukizi. 

Ikiwa hapo kesho Jumanne, Februari mosi ni maadhimisho ya mwaka mmoja tangu jeshi la Myanmar kupindua Serikali ya kiraia iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kuwaweka kizuizini kiholela viongozi wa Serikali, akiwemo Mshauri wa Serikali Aung San Suu Kyi na Rais Win Myint. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anasimama katika mshikamano na watu wa Myanmar na matarajio yao ya kidemokrasia kwa jamii jumuishi na ulinzi wa jamii zote, ikiwa ni pamoja na Rohingya. Wakati huo hii shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO limesema mwaka mmoja baada ya jeshi  kutwaa mamlaka ya kijeshi nchini humo Myanmar hali ya ajira bado ni tete. 

Na Mfuko wa Elsie wa kufadhili wanawake walioko kwenye operesheni za ulinzi wa amani, EIF, hii leo umetangaza mchango wa dola 357,000 kwa ajili ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon, UNFIL. 

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
10'40"