Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 18 Januari 2022

Jarida 18 Januari 2022

Pakua

Baadhi ya tulionayo hii kutoka Umoja wa Mataifa 

Nchini Afghanistan, majira ya baridi kali yamebisha hodi huku wakimbizi wa ndani waliosaka hifadhi kwenye mji mkuu Kabul wakihaha kujikinga na familia zao kwenye mahema yasiyo na vifaa vya kuleta joto. 

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la masuala ya Kiuchumi na Kijamii, ECOSOC Collen Vixen Kelapile ameiteua Tanzania kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Saba la Wadau Mbalimbali wa masuala ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi katika kutekeleza Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa. 

IFAD yasaidia wanawake wa Kisiwa cha Sumar nchini Ufilipino wajikomboa kiuchumi. 

Katika makala utasikia maoni na matamanio ya baadhi ya wakimbizi waliko katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda hususani kuhusu kupata makazi katika nchi ya tatu. 

Audio Duration
14'54"