Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 MEI 2021

28 MEI 2021

Pakua

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Leah Mushi anakuletea
-Leo ni siku ya kimataifa ya hedhi salama ujumbe ukiwa Hatua na Uwekezaji katika Hedhi salama, wakati huu ambapo suala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni ugonjwa au mkosi na hivyo kuwakosesha watoto wa kike haki ya kupata huduma ya kujisafi wakati wa mzunguko wa hedhi kila mwezi.

-Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma ulioko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hawana makazi hivi sasa na wako kwenye harakati za kuhama  kwa hofu ya kwamba volkano katika Mlima Nyiragongo inaweza kulipulka tena.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, leo limezindua kampeni ya kusaka kuwezesha wakimbizi vijana wenye vipaji kuweza kuendelea na elimu ya juu. 

-Mada kwa kina leo inajikita na walinda amani vijana kutoka Tanzania kikosi cha 8 au TANZBAT 8 wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa DRC  MONUSCO

-Na katika kujifunza Kiswahili katibu Mkuu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA Mwanahija Ali Juma anafafanua maana ya neno Mkafa

Audio Credit
UN News/Leah Mushi
Sauti
12'21"