Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 Mei 2021

25 Mei 2021

Pakua

Hii leo jaridani tunaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika janga la mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini.  Kisha tunaangazia ripoti ya UNICEF ya kwamba ukosefu wa maji ni silaha hatari zaidi kuliko hata mabomu kwa watoto. Nchini Tanzania kijana Aisha Kingu atumia mashairi kuelimisha watu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Makala tunarejea DRC kuangazia ziara ya Mkuu wa UNFPA katika hospitali ya Panzi jimboni Kivu Kusini na tunakunja jamvi na mashinani huko Uvinza kwa wachimba madini ya chumvi. Karibu na mwenyeji wako leo ni Leah Mushi.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'36"