Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 Mei 2021

17 Mei 2021

Pakua

Mabadiliko ya Tabia nchi yameleta athari kote ulimwenguni, miongoni mwa changamoto zilizoletwa na adha hiyo ni pamoja na ukosefu wa mvua hali inayopelekea kuwepo na uhaba wa chakula na mahali pengine mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na mazao kushindwa kustawi kabisa.

Maeneo yanayokaliwa na wakimbizi pia yanapitia changamoto hii. Makazi ya muda wanayoishi wakimbizi yanashindwa kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi hivyo shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi- UNHCR, mbali na kuhakikisha usalama wao pia linakuja na mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo. Leah Mushi ameangazia wakimbizi wa Ethiopia walioko Sudan na kutuambia ni hatua gani zinachukuliwa.

Audio Credit
Flora Nducha\Leah Mushi
Audio Duration
10'18"