Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Mei 2021

21 Mei 2021

Pakua

Kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambayo huadhimishwa kila Mei 23, mwaka huu kauli mbiu ikiwa, “haki za wanawake ni haki za binadamu! Tokomeza Fistula sasa", Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA linasema haipaswi kuachiwa wanaokubwa na wanaoathirika kutokana na tatizo hilo kwani kila mtu anahitaji maisha yenye hadhi.

UNFPA inasema tatizo la fistula ambalo husabisha tundu kubwa kati ya njia ya mkojo n ahaja kubwa kwa wanawake limetokomezwa katika nchi zilizoendelea lakini bado lipo katika nchi zinazoendelea ikikadiriwa kwamba takriban wanawake na wasichana 500,000 wanaishi na ugonjwa huo.

Moja ya nchi ambazo bado mzigo wa fistula unasalia ni Kenya. Grace Kaneiya akiwa Nairobi nchini humo ametembea hospitali ya taifa ya Kenyatta na kuzungumza na muuguzi Beatrice Oguttu ambaye anashughulikia wanawake wanaokumbwa na changamoto mbali mbali za kiafya ikiwemo Fistula.

Audio Credit
Flora Nducha/Grace Kaneiya
Audio Duration
11'