Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

16 MACHI 2021

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo  Grace Kaneiya anakuletea 

-Somalia imefuata nyayo za  nchi zingine za Afrika na kuanza kampoeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 baada ya kupokea shehena kupitia mkakati wa COVAX

-Mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa kwa mfuko wa kiamataifa wa mshikamano kwa ajili ya COVID-19 WHO inasema umefanya mambo mengi lakini inawasihi wahisani kuendelea kuutunisha 2021

Sauti
12'40"

15 Machi 2021

Jaridani Machi 15 2021 na Grace Kaneiya kwa habari kwa ufupi, makala yetu kwa kina ikiangazia mwanamke kiongozi na ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa UN-HABITAT.

Sauti
11'24"

12 Machi 2021

Hii leo jaridani Ijumaa ya tarehe 12 machi 2021 Flora Nducha anakuletea mada kwa kina ikibisha hodi huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kukutana na familia ambayo inamletea mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane baada ya kumuokoa msituni wakati wa mashambulizi kutoka kwa waasi wa kikundi cha ADF. Leo pia ni wasaa wa kujifunza Kiswahili ambapo methali isemayo La kuvunda halina ubani itamulikwa na mchambuzi wetu kutoka BAKIZA.

Sauti
11'55"

11 Machi 2021

Hii leo jaridani ikiwa ni mwaka mmoja tangu shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO litangaze ugonjwa wa Corona au COVID-19 ni janga la afya duniani, tunaanzia nchini Uganda ambako chanjo dhidi ya ugonjwa huo imeanza kutolewa kwa wahuudumu wa afya na wafanyakazi wengine muhimu walio mstari wa mbele. Tutasalia huko huko Uganda kwenye makazi ya wakimbizi  ya Bidibidi ambako walipata ugeni kutoka kwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi duniani, Filippo Grandi.

Sauti
13'13"

10 Machi 2021

Leo Jumatano ya Machi 10, 2021 Flora Nducha anaanza na ripoti kutoka Kenya ambako chanjo imeanza kutolewa dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19. Kisha anakwenda nchi jirani ya Tanzania ambako Umoja wa Mataifa kupitia kituo chake cha biashara, ITC, umeleta nuru kwa wanawake wajasiriamali wanaokamua chikichi kuwa mafuta ya mawese huko Kigoma. Kutoka Tanzania ni Sudan Kusini ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wanajenga barabara katika mazingira magumu.

Sauti
13'7"

09 Machi 2021

Hii leo jaridani Flora Nducha anamulika harakati za kuondokana na ndoa za umri mdogo duniani akimulika mtoto aliyeolewa na mzee huko nchini Bangladesh, kisha anaangazia mpango wa elimu haiwezi kusubiri ambao umepatiwa dola milioni 1 nchini Niger na mwisho ni taarifa kuhusu madereva wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakifanya kazi na Umoja wa Mataifa. Makala tunakwenda Tanzania ambako Paul Siniga, al maaruf Rio Paul anazungumzia jinsi ushiriki wake wa programu ya HeforShe umemsaidia kuwezesha kujenga usawa wa kijinsia nchini Tanzania na usisahau kuna mashinani, Karibu!

08 Machi 2021

Hii leo Jumatatu Machi Nane ni siku ya wanawake duniani na jarida letu leo limejikita na siku hiyo tukimulika wanawake katika habari yetu kwa ufupi halikadhalika mashinani. Na kwa kuwa ni jumatatu, tuna mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Tanzania kwake Ramlat Omar kijana wa kike ambaye anasimulia ni vipi amebadilika kutoka kuwa msichana hatarishi kwenye jamii yake hadi kuwa mkombozi na mjasiriamali wa kupita mlango hadi mlango kunusuru siyo tu vijana wa kike kama yeye bali pia wa kiume na vile vile wanawake kupitia mbinu alizopata kutoka shirika la kiraia la Restless Development.

Sauti
13'24"

05 Machi 2021

Hii leo jaridani ni mada kwa kina tunakwenda Tanzania ambako mhitimu wa Chuo Kikuu aweka alichosomea pembeni na kuanza kutumia kalamu ya wino kuchora picha, kulikoni? Habari kwa ufupi imesheheni taarifa kuhusu saratani, Corona na ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis nchini Iraq na leo katika kujifunza kiswhahili ni uchambuzi wa methali, Chozi la akupendaye hutoka kwenye chongo au kengeza! Karibu basi na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
15'48"

03 Machi 2021

Hii leo jaridani tunamulika siku ya usikivu wa masikio duniani halikadhalika siku ya wanyamapori duniani. Kumbuka kuwa mtu mmoja kati ya wanne yuko hatarini kupoteza uwezo wa sikio lake kusikia. Je wewe unatunza sikio lako namna gani? Kuhusu wanyamapori, wito unatolewa kutunza misitu kwani ndio makazi siyo tu ya wanyamapori bali pia ni chanzo cha bayonuai bora kwa uhai wa viumbe vyote na sayari dunia. Kisha ni TANZBATT_!3 tukimulika Sajini Mkamati yeye akionesha mchango wa wanawake katika ulinzi wa amani, katika kuelekea siku ya wanawake duniani wiki ijayo.

Sauti
11'59"