Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 Machi 2021

08 Machi 2021

Pakua

Hii leo Jumatatu Machi Nane ni siku ya wanawake duniani na jarida letu leo limejikita na siku hiyo tukimulika wanawake katika habari yetu kwa ufupi halikadhalika mashinani. Na kwa kuwa ni jumatatu, tuna mada kwa kina na leo tunakwenda nchini Tanzania kwake Ramlat Omar kijana wa kike ambaye anasimulia ni vipi amebadilika kutoka kuwa msichana hatarishi kwenye jamii yake hadi kuwa mkombozi na mjasiriamali wa kupita mlango hadi mlango kunusuru siyo tu vijana wa kike kama yeye bali pia wa kiume na vile vile wanawake kupitia mbinu alizopata kutoka shirika la kiraia la Restless Development. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'24"