Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

03 Machi 2021

03 Machi 2021

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika siku ya usikivu wa masikio duniani halikadhalika siku ya wanyamapori duniani. Kumbuka kuwa mtu mmoja kati ya wanne yuko hatarini kupoteza uwezo wa sikio lake kusikia. Je wewe unatunza sikio lako namna gani? Kuhusu wanyamapori, wito unatolewa kutunza misitu kwani ndio makazi siyo tu ya wanyamapori bali pia ni chanzo cha bayonuai bora kwa uhai wa viumbe vyote na sayari dunia. Kisha ni TANZBATT_!3 tukimulika Sajini Mkamati yeye akionesha mchango wa wanawake katika ulinzi wa amani, katika kuelekea siku ya wanawake duniani wiki ijayo. Makala tuko nchini Kenya na mashinani tunamsikia mkuu wa IMF akielezea matumaini yake kwa bara la Afrika. Karibu na mwenyeji wako leo ni Flora Nducha.

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'59"