Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 Machi 2021

04 Machi 2021

Pakua

Leo Alhamisi ya Machi 04 mwenyeji wako ni Flora Nducha na miongoni mwa aliyokuandalia hii leo ni mapendekezo kutoka Umoja wa Mataifa ya kwamba wanawake maskini katika nchi zinazoendelea wapatiwe kima cha chini cha kipato au ujira kama njia ya kuwawezesha kukabiliana na changamoto zitokanazo na COVID-19. Anamulika pia harakati za mlinda amani wa kitanzania anayehudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa huko Darfur, Sajini-Taji Felista Temba za kupatia wanawake wa Darfur stadi za ujasiriamali ikiwemo mapishi ya maandazi na kalmati. Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati hali ya usalama ikiendelea kuzorota, Umoja wa Mataifa wahaha kusaidia wakimbizi waliokimbilia nchi jirani ya DR Congo na mashinani leo tunamulika mtoto tipwatipwa huko Ugiriki ambaye bibi yake sasa anampatia mlo bora ili aondokane na hali hiyo na makala tunakutana na Bwana Christian Mwamanga kutoka Tanzania shughuli na mchango wa mradi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Karibu!

Audio Credit
FLORA NDUCHA