Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 MACHI 2021

25 MACHI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari za UN hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR laisihi serikali ya Kenya kuhakikisha maamuzi kuhusu kufunga kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab yanaheshimu haki za wakimbizi na kuwa ni suluhuhisho muafaka na endelevu

-Katika siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa katika bahari ya atlantiki Katibu Mkuu Antonio Guterres anataka kuwaenzi waathirika wa utumwa na biahsra hiyo kwa kuanika bayana historia na madhila waliyopitia na kuhakikisha yanakomeshwa

-Nchini Tanzania harakati za Umoja wa Mataifa kujengea uwezo wakulima katika kutambua mbinu bora za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, zimezaa matunda huko mkoani Kigoma baada ya wakulima wa wilayani Kakonko kuvuna zao la muhogo walilopanda kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu

-Makala leo inatupeleka Kenya kwa vijana wawili  wabunifu ambao wametengeneza roboti ya kusaidia watu wenye ulemavu.

-Na Leo mashinani tutaelekea nchini Tunisia kukutana na mfugaji mwanamke wa ngamia, ambaye sio tu amebadili maisha yake lakini pia ya wanafamilia yake

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
13'5"