Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 MACHI 2021

26 MACHI 2021

Pakua

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea

-Umoja wa Mataifa leo unapeperusha bendera zake katika Makao Makuu na mkatika ofisi zake kote duniani nusu mlingoti ili kumuenzi  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli aliyefariki dunia 17 Machi na kuzikwa leo Chato mkoani Geita Tanzania

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limefanikiwa kuwafikia wakimbizi kKaskazini mwa jimbo la Tigray Ethiopia kwa mara ya kwanza tangu Novemba mwaka jana 2020

-Shirika la mpango wa chakula duniani limesema hali ya njaa inatarajiwa kubwa mbaya zaidi nchini Angola hasa kwa kuwa taifa hilo la Kusini mwa Afrika linashuhudia ukame mbaya zaidfi kuwahi kutokea kwa miongo minne

-Mada kwa kina hii leo inatupeleka Kenya kuzungumza na Michael Macharia kuhusu tiba mpya ya Kifua Kikuu ambaye imeanza kutolewa kwa nchi sita duniani ikiwemo Kenya

-Nas katika kujifunza Kiswahili leo tunaye Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la taifa BAKITA Onni Sigalla akifafanua maana ya methali "Kanga hatagi ugenini"

Audio Credit
UN News/ Assumpta Massoi
Audio Duration
15'54"