Radio ya UN yawa kiungo cha wanafunzi na elimu wakati wa COVID-19 Sudan kusini 

20 Mei 2020

Radio Miraya inayoendeshwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMIS imekuwa chombo muhimu cha kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kupata elimu kupitia vipindi vya redio wakati huu shule zikiwa zimefungwa kutokana na janga la COVID-19 nchini .

Katika studio za Redio hiyo zilizoko mjini Juba waalimu wa masomo mbalimbali wakijiandaa kupeperusha vipindi ambavyo ndio njia pekee kwa sasa ya kuhakikisha maelfu ya watoto wanaosalia majumbani kujikinga na corona wanaendelea kusoma

Urushwaji wa vipindi hivyo umeandaliwa kwa ushirikiano wa wizara ya elimu ya Sudan Kusini na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kisha kurushwa bure na Redio hiyo ya UNMISS. Mkuu wa UNMISS ni David Shearer

Mshiriki anatoa ujumbe wake katika mjadala kwenye kipindi cha radio Sudan Kusini
UN Photo/Tim McKulka
Mshiriki anatoa ujumbe wake katika mjadala kwenye kipindi cha radio Sudan Kusini

“Hii ni fursa moja ambayo watoto wanaendelea kuwa na hamasa ya kusoma, injumuisha familia pia kwa sababu kila mtu atasikiliza kipindi hivyo ingawa shue zimefungwa , watoto wanaweza kuendelea kusoma na kuendelea na utaratibu wa shule na hamasa ya masomo.

Waziri wa elimu wa nchi hiyo Awut Deng Aculi anasema wametumia redio kwa kuwa inafika mbali na wengi wanaweza kumudu kwani

"Mfumo wa elimu umeathirika sana, tunaamini kwamba baada ya kufunga shule ilikuwa muhimu kuendelea na masomo na hii imekuwa fursa kwa watoto kuendelea kusoma wakiwa nyumbani”

Kwa mwalimu wa shule ya msingi Alfred Anasi Dominic kutumia Redio ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wake

"Nimefurahi sana kwamba tunarusha vipindi kupitia Radio Miraya kwa sababu inafikia wasikilizaji wengi nchini mwetu. Kila jimbo unakokwenda Radio Miraya inatangaza. Naamini kwamba , wasikilizaji wetu , watu wetu watafaidika sana na vipindi hivi"

Vipindi hivyo vya masomo vinarushwa mara mbili kwa siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na mbali ya kurusha vipindi vya shule radio Miraya imejiolea kurusha matangazo ya kuelimisha jamii kutwa nzima kuhusu kujikinga na virusi vya corona.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter