Vijana wabuni kifaa cha mafunzo ya sayansi kwa vitendo bila mwalimu

20 Mei 2020

Nchini Tanzania kikundi cha vijana 8 kimetengenza vifaa vinavyowezesha wanafunzi wa masomo ya sayansi kufanya mafunzo kwa vitendo bila ya kuhitaji mwalimu. 

Hapa ni Katika Eneo la Kazi .....! Ambapo Vijana wanane kutoka eneo la Ilemela Mwanza nchini Tanzania ..wakiwa na nia ya dhati kuwasaidia wanafunzi wa Shule za sekondari kupenda kujifunza masomo ya sayansi hususani katika kipindi hiki shule zikiwa zimefungwa kutokana na janga la Virusi vya  Corona COVID-19 wanaamua kuungana na kutengeneza kifaa hiki maalumu cha kujifunza sayansi kwa vitendo pasi na  uwepo wa Mwalimu.

Kevin Paul ambaye ni Mkurgenzi Mtendaji wa kikundi hiki kijulikanacho kama MITZ Group, anasema kuwa teknolojia hii imekuja kwa wasaa muafaka.

"Kifaa tulichokitengeneza tumeangazia mtaala au kitabu kinachotumika darasani kama ni mwanafunzi wa kidato za kwanza au cha pili ameshasoma baadhi ya mada darasani kifaa chetu maanake kimechukuwa hizo mada na kubadilisha kwenye mfumo wa kivitendo kwa hivyo mwisho wa siku inakuwa anafanya kile ambacho alishajifunza. Lakini hatukuishia tu kufuatilia mtaala au kitabu kinachotumika darasani tumeongezea kitabu za mwongozo au (User Guide) kwenye hii bidhaa yetu. Kwa hivyo hiyo user guide mwanafunzi mweyewe ana uwezo wa kuifuatilia bila hata msaada wa  mtu pembeni kuwa naye na hilo ndilo lengo kubwa la hiki kifaa kwamba bidhaa yetu iweze kutumika na mlengwa moja kwa moja bila hata usaidizi mkubwa kwa sababu changamoto kubwa tumeiona walimu waweza kuwa wanaruka somo la kuwafundisha maabara wanafunzi.Muda ni mwingi wa kuwaandalia vile vitendo lakini pia wanahitaji kuwepo pale ilikuweza kuwasimamia.Kama tumeweza kuandaa ule muda wa kuandaa vitendo lakini pia tumeondoa lili tatizo la uangalizi sasa hivi mwanafunzi mwenyewe sasa  ukimpaa kitabu cha  nadharia na hiki kifaa anakuwa amemaliza nadharia na vitendo (Theory na practical) yeye mwenyewe." 

Pamoja na kuonyesha nafasi ya ubunifu huu, Kevin anaamini kutokana na utafiti waliofanya  kifaa hiki kina nafasi kubwa hususani katika kuibua vipaji vya wanasayansi wenye weledi mzuri kuanzia ngazi za elimu ya sekondari tofauti na miaka iliyopita...

"Wanahitaji msaada mkubwa sana wa kuweza kueleweshwa kwa vile anaweza kuwa anajiona kwamba hahitaji kufanya somo la sayansi kwasababu elimu aliyofundishwa ya sayansi haikuwa katika hali ya kupendezeka au hali ya kuvutia kwa hivyo anaamua asiendelee na sayansi kwasababu aliona kama haina maana. Wanaongea maneno kama wanavyoongelea masomo ya sanaa kwa hivyo vifaa vyetu sisi vinalenga eneo hilo ili kuweza kuwaunganisha walio katika kuelekea kuacha sayansi ili wakienda kidato cha tatu tuwe na wanafunzi wengi wa sayansi."

Swali ni Je Kifaa hiki kinafanyaje kazi? Mwanafunzi anafanyaje?

"Sasa hapa unatakiwa uunganishe katika mfumo huu kwa hivyo cha kufanya sasa ni kuweza kuangalia kipi kinaanza tukianza na hii hapa tunaweka labda hapa hivi alafu tunakija hii hapa inakaa hapa katikati alafu unakuja kwa hii LED tukaweka hapa alafu hii swichi tukaiweke hapa kwa hivyo sasa mwisho wa siku nataka tuunganishe hizi nayo hapa tunaweza kufanya hivi hii na hii hapa."

METZ Group wanauza kifaa hiki kwa  Shilingi za Kitanzania 30000 sawa na Dollar 12 za Marekani ambapo Kelvin anasema wameazimia kutanua soko lao hata kwa ngazi ya juu zaidi na shule za msingi pia, "Lakini pia kwa sasa hivi janga ambalo limetokea tunachokifanya ni kwamba vitendo(pratical)hizo hizo ambazo vinafanyika kitando cha kwanza na cha pili nyingi ni zile za kuanzia darasa la tano mpaka la saba kinachotofautiana ni lugha au ule upana wa kuweza kuelezea kitu hicho.Kitu ambacho tunabadilsha sasa hivi ni masomo haya ya vitendo tunabadili iliiendane na ule upana wa mahitaji ya mtaala wa darasa la tano hadi la saba.Lakini pia tunapangia tunabadilisha kitabu za mwongozo au (User Guide)kiwa katika lugha ya kiswahili iliiweze kuwahusisha na kuwajumuisha watoto wa shule za kawaida za kata na zile za msingi za serikali." 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter