Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 Mei 2020

22 Mei 2020

Pakua

Leo Ijumaa tuna mada kwa kina tunamulika ukatili unaofanyika majumbani kutokana na zuio la kutoka nje lililowekwa kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya Corona au coronavirus">COVID-19. Tunakwenda wilaya ya Hoima nchini Uganda, wanawake wanalalama, wanaume halikadhalika, ndani hakukaliki, na msemo wa "nyumba ni sufuria" umeshamiri. Tutakuwa na muhtasari wa habari ukibisha hodi Kairobangi na Ruai nchini Kenya, tutaenda Bangladesh na leo neno la wiki tunamulika methali na mchambuzi wetu anatoka Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'22"