Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 05 2020

25 05 2020

Pakua

Katika Jarida maalum la habari hii leo Flora Nducha anakuletea

Leo ikiwa ni siku ya Afrika Umoja wa Mataifa umelisihi bara hilo na nchi zinazofanya uchaguzi kudumisha demokrasia wakiendesha uchaguzi huo hata wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19

 

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet, umebaini kusambaa kwa ugonjwa wa saratani ya koo na sababu kuu ikiwa ni uwepo wa mashine za uchunguzi zinazofanya uchunguzi kupita kiasi hususan katika nchi za kipato cha kati.

 

Nchini Sudan Kusini, mtandao wa wanawake wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, unaoongozwa na polisi wa Umoja wa Mataifa, UNPOL, umesambaza barakoa 250 kwa viongozi wa kijamii kwenye kituo cha ulinzi wa raia mjini Wau.

 

Mada yetu kwa kina leo inajikita na hatua zinazochukuliwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP nchini Tanzania katika vita dhidi ya COVID-19

Na mashinani tunaelekea Congo DRC utamsikia binti ambaye yeye na mama yake walibakwa kijiji chao kiliposhambuliwa na waasi.

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
9'57"