27 MEI 2020

27 Mei 2020

Kwenya Jarida la Umoja wa mataifa hii leo
-COVID-19 yawa upenyo wa kutangaza maziwa ya kopo badala ya maziwa ya mama
-Tutasikia kauli ya mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jinsi COVID-19 imebadilisha maisha ya familia yake.
-Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imekuwa faraja kwa wengine: tutasikia kutoka kwa Fundi Beatrice kutoka Tanzania anyeshona barakoa.
-Na kwenye mashinani leo tutakwenda nchini Uganda kuangazia harakati za  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF katika kusambaza miundombinu rafiki ya maji safi na salama.
-Kwenye Makala tutaangazia mwanamke mjasiriamali ambaye ametumia uzoefu wake wa ufundi cherehani kama njia ya kupunguza madhara ya COVID-19 kwa pato lake.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
12'31"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud