Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 Mei 2020

29 Mei 2020

Pakua

Kwenye Jarida la Umoja wa Mataifa leo ni siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa duniani :

-kwenye mada yetu ya kina baadhi ya wanawake wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wameomba walinda amani wanawake kutoka Tanzania waendelee kuwaunga mkono kiuchumi na kijamii.

-Mlinda amani mwanamke kutoka Tanzania ambaye anahudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO amethibitisha umuhimu wa uwepo wa askari wa kike katika ulinzi wa amani

-UNHCR na wadau wengine wa misaada wanaongeza juhudi za msaada kwa wakimbizi wa ndani zaidi ya 4,000 ambao wamepoteza kila kitu kutokana na moto mkubwa ulioteketeza kambi ya wakimbizi wa ndani mjini Maiduguri jimbo la Borno nchini Nigeria.

-Na dola bilioni 2.4 zinahitajika katika miezi saba ijayo, ili kuendelea kutoa msaada wa kibinadamu na kuokoa maisha ya watu milioni 19 walioathirika na miaka mitano ya vita , kutawanywa, utapiamlo, magonjwa na mfumo wa afya kuwa katika shinikizo kubwa kutokana na janga la COVID-19.

-Na leo kwenye neno tunaangazia maana za neno "VUVIA" 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'56"