Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 MEI 2020

26 MEI 2020

Pakua

Katika Jarida maalum la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Walinda amani wawili wanawake mmoja kutoka Brazili na mwingine kutoka India wameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mchagizaji wa masuala ya kijinsia kwa mwaka 2019. Wanajeshi hao Meja Suman Gawani kutoka India na kamanda Carla Monteiro Araujo kutoka Brazili watakabidhiwa tuzo hiyo Ijumaa ya 29 Meisiku ya walinda amani duniani.

-Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa mataifa yote kuwasaidia wahamiaji na familia zao wakati na baada ya janga la virusi vya corona au COVID-19 bila kujali hadhi ya uhamiaji wao

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, leo limesema linahitaji dola milioni 878 ili kuendelea kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa mamilioni ya raia wa Yemen wanaohitaji msaada wa kibinadamu ili kuishi.

-Mada yetu kwa kina leo inamulika athari za janga la COVID-19 kwa maisha ya watu nchini Kenya

-Na mashinani tuko DRC congo kusikia ujumbe wa kujikinga na Corona kutoka kwa mtoto wa miaka 9.

Audio Credit
UN News /Flora Nducha
Audio Duration
9'57"