Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

20 FEBRUARI 2024

Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kijamii Duniani. 

Jarida linaletwa kwako na LEAH MUSHI na kubwa hii leo ni mada kwa kina kutoka nchini Kenya ambako serikali na wadau wa wanyamapori wamechukua hatua kulinda moja ya Wanyama walio hatarini kutoweka , Faru. 

Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani. 

Karibu. 

Sauti
13'11"

19 FEBRUARI 2024

Mgogoro wa Sudan ni tishio kwa ukanda mzima huku njaa ya utapiamlo vikiongezeka WFP imeonya.

Maelfu ya watu wayakimbia machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Makala: UNICEF na UNFPA waungana kutokomeza ndoa za utotoni nchini Nepal.

Mashinani : Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini Jean-Pierre Lacroix afanya ziara kutatathimini hali.

Sauti
10'