Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 APRILI 2024

22 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya hali ya joto dunianina madhara yake kwa afya na wafanyakazi, Naomi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa ndani DR Congo. Makala tunakupeleka nchini Sudan na mashinani nchini Sudan Kusini, kulikoni? 

  1. Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
  2. Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao.  
  3. Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa.
  4. Na mashinani tutapeleka Tambunra nchini Sudan Kusini kumsikia mkimbizi wa ndani akisihi kurejea kwa amani illi aweze kurudia nyumbani.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
12'