Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 APRILI 2024

26 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mzozo nchini Sudan, na jinsi amabvyo mzozo huo unavyathiri wanawake. Makala tunaangazia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za watu wa asili na mashinani usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi nchini Kenya. 

  1. Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.
  2. Na tukisalia nchini Sudan, mwaka mmoja wa mzozo umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito.  
  3. Katika makala Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.
  4. Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanahaha kushughulikia changamoto za usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
12'8"