Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF/Henry Bongyereirwe

Hakuna uzuri wowote wakushiriki ngono katika umri mdogo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto -UNICEF nchini Uganda linafadhili mradi wa Mama kwa Mama ambao unajengea uwezo maafisa wa ustawi wa jamii wanaopita kila kaya maskini kusaka  barubaru na vijana balehe waliopata mimba katika umri mdogo na kuwapatia stadi za ufundi ili  hatimaye waweze kujipatia kipato na kubadilisha maisha yao. 
(Taarifa ya Leah Mushi) 
 

Sauti
1'52"
© ILO

Wahamiaji wa kimataifa waongezeka kutoka Milioni 164 mpaka 169

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shjirika la kazi duniani ILO inakadiria kwamba kati ya mwaka 2017 na 2019 idadi ya wahamiaji wa kimataifa imeongezeka kutoka milioni 164 hadi milioni 169, sanjari na kuongeza idadi ya wafanyakazi wahamiaji. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Makadirio ya kimataifa ya ILO kuhusu wafanyakazi wahamiaji:matokeo na mfumo” inaonyesha kwamba mwaka 2019 wanayakazi wahamiaji wa kimataifa walikuwa karibu asilimia 5 wa wafanyakazi wote duniani na kuwafanya kuwa chachu muhimu ya uchumi wa dunia. 

Sauti
2'50"
@Yak

Jukwaa la Usawa wa Kijinsia aanza rasmi huko Paris Ufaransa

Hii leo huko Paris nchini Ufaransa kumeanza jukwaa la siku tatu la kusaka kusongesha usawa wa kijinsia kwa kujumuisha vijana katika kufanikisha lengo hilo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huo unafanyika kwa kuzingatia kuwa miaka 25 baada ya mkutano wa kimataifa wa wanawake huko Beijing nchini China, bado usawa wa jinsia unasalia ndoto kwa maeneo mengi.  
 

Sauti
3'36"
© WFP/Arete/Fredrik Lerneryd

Biashara ya sabuni inaendesha maisha yangu; Mjane nchini DRC

Katika jimbo la Tanganyiko huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mizozano baina ya jamii ya mji wa Kabalo sasa imesalia historia baada ya miradi ya uwezeshaji amii inayotekelezwa na mashirika ya  Umoja wa Mataifa kuleta siyo tu utengamano bali pia kuinua vipato vya wanajamii wakiwemo wajane. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Flora Nducha)

Sauti
4'4"
© UNICEF Moldova

Rais wa Tanzania atoa takwimu za wagonjwa wa COVID-19

Wakati shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika likionya kuwepo kwa wimbi la tatu la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 barani Afrika, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema sasa taifa hilo lina wagonjwa zaidi ya 100 na tayari taratiu zinafanyika ili kuingia chanjo ya COVID-19.
Rais Samia amesema hayo Jumatatu juni 28 2021 wakati akijibu swali wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es salaam.

Sauti
2'16"
© UNHCR/Santiago Escobar-Jarami

UNHCR yazishukuru nchi za Panama, Ecuador na Colombia

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya wiki ya kutembelea nchi zilizoko Amerika ya Kusini na kuzishukuru nchi hizo kwa kazi kubwa ya kuhifadhi wakimbizi ambapo takwimu zinaonesha wamehifadhi zaidi ya robo ya wakimbizi wote duniani.

Takwimu za dunia zinaonesha kuna wakimbizi zaidi ya milioni 82 na asilimia 20 ya wakimbizi hao wamepewa hifadhi kwenye nchi za Panama,Colombia na Ecuador. 

Sauti
1'51"