Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yawatumia viongozi wa dingi kuhamasisha kampeni ya chanjo ya COVID-19 Garissa

UNICEF yawatumia viongozi wa dingi kuhamasisha kampeni ya chanjo ya COVID-19 Garissa

Pakua

Janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiendelea kutikisa dunia huku taarifa potofu kuhusu chanjo zikiendelea kusambaa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo na faida zake katika kuepusha kusambaa zaidi kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. Taarifa ya John Kibego inafafanua zaidi.
(Taarifa ya John Kibego)
Nats..
Tuko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya waumini wa madhehebu ya kiislamu wakiingia msikitini tayari kwa ibada wakati huu ambapo gonjwa la Corona bado linaendelea kuleta shaka na shuku.
Kama mbinu ya kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeshapeleka dozi milioni 21 za chanjo dhidi ya Corona na linasaidiana na Wizara ya afya kuhakikisha watu wanachanjwa.

Hata hivyo kuna changamoto ya taarifa potofu kuhusu chanjo na ndipo UNICEF ikashirikisha viongozi wa dini akiwemo Sheikh Omar Dagane, Imán wa msikiti hapa Garissa.
(Sauti ya Sheikh Omar Dagane)- Jongo
“Kama Imam wa jamii hii niña wajibu wa kushauri jamii kuhusu suala lolote la maslahi yao. Leo nimewaeleza waumini umuhimu wa kujikinga na COVID-19 kwa kupata chanjo. kupata chanjo ili kujikinga na COVID-19. Nimenukuu moja ya kauli za Mtume Muhamad SAW alipoulizwa na mfuasi wake iwapo amfunge kamba ngamia wake ambapo jibu lilikuwa Muamini Mungu lakini funga ngamia wako. Na vivyo hivyo tunapaswa kumuamini Mungu lakini tupate chanjo, vaa barakoa, nawa mikono, ili kujikinga.”

Baada ya mahubiri mmoja wa washiriki Isak Abidi akafunguka akisema, “Nimesikiliza mahubiri ya Imam na ujumbe wa afisa wa afya na sasa nimeamua kuwa nakwenda kupata chanjo.”
Abdullahi Abagira ni afisa wa UNICEF kaunti ya Garissa na anasema COVID-19 imekuwa na madhara ya aina mbalimbali hususan kwa watoto na hivyo UNICEF imesaidia kwa kusambaza siyo tu chanjo bali pia kufanikisha uwepo wa wahudumu wa afya wa kutoa huduma hizo.
 

Audio Credit
UN News/Kibego-Stringer
Audio Duration
2'12"
Photo Credit
John Kibego