Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

WFP/Rein Skullerud

Wanafunzi na wazazi wanufaika na mradi wa WFP wa chakula shuleni

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP nchini Rwanda, linaendesha programu ya chakula kutoka nyumbani kwenda shuleni, programu ambayo inatekeleza malengo 6 ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba 2 la kutokomeza njaa na hivyo kuwaacha wazazi na wanafunzi wakiwa na furaha. Leah Mushi ana taarifa zaidi.
 
(Taarifa ya Leah Mushi)
Programu ya kuwapatia wanafunzi mlo shuleni inatekelezwa katika nchi nyingi duniani na pengine huwa unajiuliza chakula hicho kinatoka wapi?
 

Sauti
2'5"
Photo: OCHA Burundi / Ana Maria Pereira

Watafiti wakifanya kazi kwa pamoja na kushirikiana na sekta nyingine, maendeleo ya wananchi yatapatikana

Mkutano unaohusu utafiti, sayansi teknolojia na uvumbuzi katika kukuza ushirikiano na maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni sehemu ya mbio za kuyafikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, ulioandaliwa na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia ya Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu umehitimishwa leo jijini Bunjumbura kwa kunuia kuwapa nafasi watafiti katika kukuza uchumi.

Sauti
1'52"
Picha na UNICEF/Vockel

Mkimbizi wa DRC aeleza alivyojikombia kiuchumi

Kutana na mkimbizi Felicitee Anibati kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ambaye kwa sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu nchini Sudan Kusini , ni mama, mkulima na mjasiriamali mwenye mafanikio ambaye sasa anatumia mafanikio yake kuwasaidia wanawake wenzie ili kufika alipo yeye. Flora Nducha anasimulia zaidi

Sauti
2'9"
© Unsplash

Dunia bado ipo hatarini kuwa na ongezeko la joto : UNEP

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP imeeleza kuwa ahadi mpya na zilizorekebishwa kuhusu viwango vya nchi vya kukabili mabadiliko ya tabianchi, NDCs hazijafikia lengo lililowekwa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi na hivyo ulimwenguni kuwa hatarini kuwa na ongezeko la joto la angalau nyuzijoto angalau 2.7 katika karne hii
 
(Leah Mushi na taarifa zaidi.)

Sauti
1'17"
UNICEFBurundi/2021/Ruben Hamburger

Ng'ombe mmoja huko Burundi akomboa familia iliyokuwa taabani

Mtamba mmoja wa ng’ombe anaweza kuonekana si chochote kitu kwa wafugaji wabobezi lakini kwa Beatrice Nibogora na familia yake nchini Burundi, mtamba huyo akipatiwa jina Maza amegeuka lulu na ufunguo wa maisha yenye matumaini na kutimiza methali ya wahenga ya kwamba baadhi ya dhiki ni faraja.

Hii ni baada ya mradi wa Benki ya Dunia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kubisha hodi kunusuru kaya maskini. Anold Kayanda anafafanua zaidi.

(Taarifa ya Anold Kayanda)

Sauti
1'58"
© UNICEF/Helene Sandbu Ryeng

Mafuriko yawatenga wananchi kwa miezi 6 bila msaada wowote nchini Sudan Kusini

Mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha miezi 6 iliyopita nchini Sudani Kusini zimeathiri miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege huku zaidi ya wakazi  700,000 wa kaunti ya Maban jimboni Jonglei wakisalia wakiiishi bila kupata msaada wowote kutokana na eneo lote kujaa maji.
Wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR kwa kutumia helipokta wameweza kufika eneo hilo na Leah Mushi anatuletea taarifa kamili.

MONUSCO

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama

Muda wa kurudisha nyuma saa ya haki za wanawake umepita, sasa iende mbele- Guterres alieleza Baraza (OVERNIGHT)
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu.  Flora Nducha na maelezo zaidi.

Sauti
3'18"